08.21.08
Posted in Sifa at 12:08 pm by Administrator
Rachel Marlon
Katika familia ya Mzee Mohamedi
ni mtoto wa tatu (3) kuzaliwa
Yesu akaniita nimtumikie. Baada
ya kuokoka nilijiunga na huduma
ya kuombea wagonjwa BCIC
Mbezi Beach huku moyoni nikiwa
na msukumo ulioendelea na
kujikuta natunga nyimbo na
hatimaye nimekamilisha albamu.
Albamu hii inaitwa “nipige chapa”
ambayo itazinduliwa tarehe 5
Octoba 2008 Diamond Jubilee na
itasindikizwa na waimbaji kama
vile Bahati Bukuku, Boniface
Mwaitege, Christina Shusho,
Upendo Nkone, Jackson Benty,
DJC, Tina Marego, Victor Arone,
Lwiza Jonasi, Ambwene
Mwasongwe na wengine wengi
sana…
Permalink
Posted in Sifa at 12:07 pm by Administrator
Sara Magesa na Queen Mtomvu, waimbaji wa nyimbo za Injili ambao wanaabudu BCIC Temeke. Wamekuwa wakiimba kwa kupokezana iwe ni kwa kusifu au kwa kuabudu ndani ya ukumbi wa PTA, waimbaji hawa wamekuwa ni vyombo vitakatifu vya Bwana Yesu kwa kazi maalum…
Permalink
08.20.08
Posted in Sifa at 12:15 am by Administrator
Karibuni Watanzania, Waafrika na Dunia nzima kwa ujumla wake kuungana nasi katika kuijulisha dunia Mungu anavyowatumia watumishi wake kulihubiri neno lake kwa njia mbalimbali
Iwe ni kwa njia ya uimbaji, tutakujulisha; kuanzia maisha ya mtumishi, mafanikio na matatizo anayokutana nayo kiutumishi. Na je, Mungu amemfanikishaje kuuangusha mlima uliokuwa mbele yake.
Tunapenda kupata maoni yako, ushari na kuwaeleza watu nini unachojua au na wengine hawakijui au ambalo ungependa kuwashirikisha wengine
Pia kwa sasa unaweza kutumia namba hii 0714 116 229 kubadilishana mawazo zaidi.
Permalink